1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu 50 wauwawa katika mashambulio ya mabomu.

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnA

Nchini Iraq , mabomu matatu yaliyolipuliwa katika magari katika eneo la kati la mji wa Baghdad yameuwa kiasi watu 50 na kuwajeruhi wengine kadha.

Polisi wanasema kuwa wanatarajia idadi ya watu waliokufa kupanda kutokana na milipuko hiyo.

Katika tukio tofauti, watu 18 wameuwawa wakati lori lililokuwa likienda kasi lilipogonga kundi la watu waliokuwa wakisubiri basi katika kituo cha basi cha Al-Wahada, kiasi cha kilometa 35 kusini mwa Baghdad.

Dereva wa lori hilo , ambaye alijaribu kukimbia , amesema kuwa breki katika gari hilo zilishindwa.

Kiasi watu tisa waliuwawa katika matukio mengine ya ghasia karibu na mji mkuu Baghdad.

Wakati huo huo Itali imekamilisha kuwaondoa wanajeshi wao wanaokadiriwa kufikia 3,000 kutoka Iraq wiki kadha kabla ya muda uliopangwa.

Wakati wa kampeni za uchaguzi , waziri mkuu wa Italia Romano Prodi aliahidi kuyaondoa majeshi ya nchi hiyo kutoka Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.