1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu kiasi ya 30 wauawa nchini Irak

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCx9

Watu kiasi ya 30 waliuawa jana nchini Irak katika matukio mbali mbali. Mtu aliojitoa mhanga aliripua gari lililokuwa na bomu na kuwauwa watu takriban 23 katika mji mkuu wa Irak, Baghdad. Miongoni mwa waliouawa 19 ni watoto. Watu wengine 19 walijeruhiwa baadhi yao wakiwa katika hali mahatuti. Shambulio hilo lilivizia watu waliokuwa wakisherehekea arusi. Kwa uchache watu wengine 7 waliuawa katika matukio mbali mbali nchini Irak kulingana na polisi.