1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu sita wauwawa, wanajeshi watatu wa Marekani pia wauwawa.

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdZ

Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limeua karibu watu sita katikati ya mji wa Baghdad. Polisi wamesema kuwa watu kadha pia wamejeruhiwa katika mlipuko huo, ambao ulitokea saa chache baada ya kumalizika kwa marufuku ya kutotembeza magari, hatua iliyochukuliwa kabla ya mchezo wa fainali kati ya Iraq na Saudi Arabia.

Ushindi wa Iraq katika mchezo huo wa kombe la mataifa ya Asia ulizusha shamra shamra kubwa katika mji huo mkuu, huku risasi zikifyatuliwa hewani licha ya marufuku iliyowekwa na serikali.

Polisi mjini Baghdad na mji wa Kut wameripoti kuwa kiasi cha watu saba wameuwawa na zaidi ya 50 wamejeruhiwa kutokana na risasi zilizofyatuliwa hovyo.

Wakati huo huo , jeshi la Marekani limesema kuwa wanajeshi wake watatu wameuwawa katika mapigano katika jimbo la Anbar magharibi ya mji mkuu Baghdad.