1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu takriban 20 wauwawa kwenye shambulio la bomu

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz5

Watu takriban 20 wameuwawa na wengine 15 kujeruhiwa wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha alipojilipua katika mji wa kikurdi karibu na mpaka wa Irak na Iran. Mlipuko huo umetokea mjini Mandali katika wilaya ya Diyala.

Sambamba na taarifa hiyo, polisi wa Irak wanasema wameipata maiti ya mwanamme mmoja aliyekuwa amevaa sare inayofanana na mavazi ya jeshi la Marekani ikielea kwenye mto wa Euphrates huko Musayyib, yapata kilomita 60 kusini mwa mji mkuu Baghdad.

Hayo yametokea huku wanajeshi watatu wa Irak wakiendelea kuwatafuta wanajeshi watatu wa Marekani waliotekwa nyara mnamo tarehe 12 mwezi huu, wakati kikosi chao kiliposhambuliwa karibu na Mahmoudiya.

Kufikia sasa jeshi la Marekani halijatoa matamshi yoyote kuhusu kisa hicho.