1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:50 wauawa wakishangilia wa timu ya soka ya Iraq

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfE

Watu 50 wameuawa na wengine zaidi ya 130 wamejeruhiwa huko Baghdad, kufuatia mashambulizi ya mabomu kwenye kundi la watu waliyokuwa wakisherehekea ushindi wa timu ya mpira wa miguu ya Iraq.

Timu hiyo ya Iraq ilipata ushindi dhidi ya Korea Kusini katika michuano ya kombe la Asia huko Indonesia.

Watu 30 waliuawa katika wilaya ya Mansour na wengine 20 katika kituo cha ukaguzi mashariki mwa Baghdad baada ya washambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika makundi ya watu waliyokuwa wakishangilia ushindi huo.

Maelfu ya watu waliingia mitaani kushangilia ushindi huo bila kujali tofauti zao za kikabila, katika tukio hadimu nchini Iraq.