1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Al Malik ataka Marekani kutoitumia kampuni iliyotimuliwa

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOE

Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al-Malik ameiuataka ubalozi wa Marekani nchini humo kuacha kuitumia kampuni ya ulinzi ya kimarekani iliyopigwa marufuku ya Blackwater.

Kampuni hiyo ilipigwa marufuku kuendesha shughuli zake nchini humo kufuatia mauaji ya watu kumi jumapili iliyopita yaliyofanywa na walinzi wa kampuni hiyo.

Waziri Mkuu huyo wa Irak amesema kuwa hatokubali kuona wananchi wa nchi hiyo wanauawa kikatili.

Rais Ggeorge Bush wa Marekani inaarifiwa kuwa ameguswa na kitendo cha walinzi wa kampuni hiyo, lakini amekataa wito wa kuiondoa kampuni hiyo nchini Irak.