1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Bomu lililotegwa ndani ya gari lauwa watu 10

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2E

Polisi nchini Irak imetoa taarifa ya kuuwawa watu 10 baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka nje ya benki katika mji wa Suweira kusini mashariki mwa Baghdad mji unaoishi jamii kubwa ya Washia.

Wakati huo huo mabomu mawili yamelipuka kando ya barabara katika mji mkuu wa Baghdad, polisi mmoja ameuwawa na wengine saba wamejeruhiwa.

Jeshi la Marekani limesema askari wake watatu zaidi wameuwawa.

Gazeti la Los Angeles Times la Marekani limeripoti kuundwa kwa tume maalum ya bunge la nchi hiyo itakayotoa mapendekezo ya mabadiliko ya mpango wa Irak kwa mwaka ujao kufuatia hali mbaya ya usalama nchini humo.