1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Iran kuandaa mkutano wa usalama

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNZ

Majeshi ya Marekani na Iraq yamewaua wanamgambo 10 wanaoshukiwa na kukamata silaha katika msako wa siku tatu zilizopita kwenye Mkoa wa Diyala.Watu hao 10 waliuawa siku ya Jumatatu katika eneo la Muqdadiyah lililo na Wasunni wengi.

Wengine watano walikamatwa na kuzuiliwa katika operesheni hiyo.Wanajeshi walivumbua zaidi ya guruneti 50,vifaa vya kutengeza bomu vilevile lori moja lililoibwa lilokuw ana shehena ya baruti kali.Silaha nyingine ambazo ni risasi na makombora zilipatikana siku hiyohiyo katika mji mkuu wa Diyala wa Baqouba.

Wakati huohuo Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki anaalika mataifa jirani na mataifa yaliyoendelea ulimwenguni katika mkutano wa kujadilia masuala ya usalama mjini Baghdad wiki ijayo.

Mkutano huo unaazimia kuimarisha uhusiano vilevile kuunga mkono juhudi za serikali yake.Kikao hicho kinatarajiwa kuwezesha mazungumzo kufanyika kati ya Marekani ,Syria na Iran.Marekani kwa upande wake inadai kuwa Syria na Iran zinachochea ghasia nchini Iraq jambo wanaolokanusha.

Mkutano huo huenda ukawahusisha maafisa wa ngazi za juu.Iran kwa upande wake inatathmini pendekezo la Marekani la kuhudhuria mkutano huo.