1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Iraq yahirisha kuwanyonga wasaidizi wa Saddam

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdM

Iraq imeahirisha kunyongwa kwa wasaidizi wawili wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein mpaka jumapili.

Wasaidizi hao, ndugu wa Saddam ambaye alikuwa mkuu wa usalama Barzan Ibrahim al-Tikrit na aliyekuwa jaji mkuu wa mahakama ya kimapinduzi, Awad Ahmed al-Bandar walipangwa kunyongwa leo.

Katibu Mkuu mpya wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon na Kamishna mkuu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu Louise Arbor wamemuomba Rais wa Iraq Jalal Talaban kutowanyonga watu hao.