1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mashambulio ya mabomu yaendelea kuua raia Iraq

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2J

Kundi lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Alqaeda nchini Iraq limesema linawashikilia wanajeshi watatu wakimarekani waliotekwa nyara jumamosi.

Matamshi hayo yametolewa huku wanajeshi wakimarekani kiasi cha 4000 wakiendeleza opresheni ya kuwatafuta wanajeshi hao waliotoweka kusini mwa mji wa Baghdad.

Wakati hayo yakiendelea umwagikaji wa damu bado unaendelea.Watu zaidi ya 60 waliuwawa hapo jana na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mashambulio mawili ya mabomu ya kutegwa ndani ya gari.

Katika eneo la kaskazini linalokaliwa na wakurdi mshambuliaji wakujitoa muhanga aliwauwa kiasi cha watu 50 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 70 kwa kujiripua ndani ya gari lililokuwa limesheheni miripuko mjini Mahmur.

Katika mji mkuu Baghdad gari lililokuwa limeegeshwa karibu na soko la Sadriyah liliripuka na kuua watu takriban ya 11 na kujeruhi wengine 43.