1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad:Mashambulio ya ndege za Marekani yauwa kiasi ya 50 mjini Sadr.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dn

Hujuma za ndege za kijeshi za Marekani asubuhi ya leo katika mji wa Sadr nchini Irak. zimewauwa kiasi ya watu karibu 50 na kuwajeruhi wengine kadhaa. Msemaji wa jeshi la Marekani alisema wanajeshi wao walikua wakiwaandama waasi ambao wanaamini wamehusika na kutekwa nyara wanajeshi wa Marekani.Ingawa alisema hakuna ushahidi kwamba raia ni miongoni mwa waliouwawa au kujeruhiwa, hata hivyo polisi ya Irak imesema wanawake na watoto ni miongoni mwa waliouawa. Mji wa Sadr ni ngome ya wanamgambo wa Mehdi waliyo watiifu kwa Kiongozi wa kidini Moqtada al-Sadr na kimegeuka kituo cha mapigano ya mara kwa mara kati ya majeshi ya Marekani na wanaharakati wa kishia.