1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mauaji yaendelea kote Iraq

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuj

Zaidi ya watu 60 waliuwawa kwenye mashambulio yaliyofanyika katika sehemu mbali mbali nchini Iraq hapo jana.

Kwa mujibu wa Polisi nchini humo shjambulio la kombora dhidi ya uwanja wa mpira katika mji wa Sadr huko Baghadad lilisababisha kuuwawa kwa kiasi watu wanane wengi wakiwa ni raia na wengine 20 wakajeruhiwa.

Kusini mwa Baghadad huko Mahmoudiyah watu sita waliuwawa kufuatia shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari lililofanywa kwenye soko.Watu wengine 16 waliuwawa kwenye matukio ya mashambulio ya risasi na mabomu kwenye mkoa wa kaskazini huko Diyala.wakati huo huo wanajeshi wa Marekani wamefahamisha kuwauwa watu 14 wanaoshukiwa kuwa waasi wa Alqaeda na wengine 48 wamekamatwa.wanajeshi hao pia wamemkomboa polisi mmoja wa Iraq aliyetekwa nyara hivi karibuni.