1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mauaji zaidi Iraq

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzS

Watu 25 wameauawa na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka nje ya soko mjini Baghdad.Wengi wa waliyouawa na kujeruhiwa ni wanawake na watoto.

Katika shambulizi lingine mashariki mwa Baghdad, wanafunzi 12 waliuawa na wengine 28 kujeruhiwa.

Aidha polisi wawili wa Iraq waliuawa baada ya kushambuliwa na mtu aliyekuwa na bunduki huko Khadra, ambapo mjini Baghdad polisi mmoja alikufa baada gari waliyokuwa nayo kutupiwa bomu.

Wakati huo huo majeshi ya Marekani yamesema kuwa yamewaua wanamgambo tisa na kufanikiwa kuwaokoa mateka 12 wa kiiraq waliyokuwa wametekwa.