1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Nour al Maliki apata pigo lingine

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbR

Waziri Mkuu wa serikali ya kishia ya Iraq, Nour al Maliki amepata pigo lingine baada ya mawaziri wanne zaidi kutangaza kususia vikao vya baraza la mawaziri.

Wiki iliyopita kundi kubwa la mawaziri wa upande wa wasunni lilijiondoa serikalini kutokana na waziri mkuu huyo kushindwa kutimiza matakwa yao yakiwemo ya kupewa usemi mkubwa katika masuala ya kiulinzi.

Wakati huo huo takriban watu 28 wameuawa katika shambulizi la kujitoa mhanga katika mji wa Tal Afar uliyoko kaskazini mwa Iraq.

Kwengineko askari wanne wa Marekani wameuawa wakati waliposhambuliwa na bomu huko katika jimbo la Diyala.Duru za jeshi la Marekani zimesema kuwa askari wengine 12 wamejeruhiwa.