1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Rais wa Iraq augua

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOT

Rais wa Iraq Jalal Talabani yuko mjini Aman Jordan kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua maradhi ya kuishiwa nguvu.

Hata hivyo serikali ya Iraq imesema hakuna haja ya kuwepo wasiwasi wowote kwani rais huyo yuko katika hali nzuri.

Rais Talabani alipata hali hiyo kutokana na kazi ngumu aliyofanya katika siku kadhaa zilizopita.Kwa mujibu wa Mwanawe kwa sasa yuko salama na anaweza kutembea.