1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Shririka la kutetea haki za binadamu lasema kesi ya Saddam haikuendeshwa vyema

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCr1

Kundi linalo tetea haki za binadamu la shirika la kimataifa la Human Rights Watch limesema kwamba kesi ya aliyekuwa rais wa Irak Saddam Hussein haikuendeshwa vyema na kwamba uamuzi wa kesi hiyo hauna msingi.

Saddam Hussein alihukumiwa kifo tarehe 5 mezi huu wa Novemba baada ya kupatikana na hatia ya kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.

Kubndi hilo limesema kuwa limeorodhesha makosa mengi ya kisheria yanayo dhihirisha kuwa Saddan Hussein hakutendewa haki katika kesi dhidi yake.

Wakili wa bwana Saddam Hussein amefahamisha kuwa hadi sasa amewekewa vikwazo kadha wa kadha ili asiweze kuwasilisha rufani dhidi ya adhabu ya kifo inayomkabili kiongozi wa zamani huku zikiwa zimebakia wiki mbili kabla ya muda wa kuwasilisha rufani hiyo kumalizika.

Serikali ya Irak imepuuza ripoti hiyo ya shirika la kutetea haki za binadamu na kusema kuwa kesi ya Saddam Hussein iliendeshwa kwa njia ya haki na usawa.