1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Umwagaji damu waendelea nchini Iraq.

31 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxJ

Kiasi cha polisi wa Iraq 16 na raia wameuwawa katika bomu lililoripuka nchini Iraq.

Magharibi mwa Baghdad mapigano yameripotiwa kati jeshi la Iraq na polisi ambao walipambana na wanamgambo katika wilaya ya al-Khadraa.

Maiti nyengine tano ambazo hazikutambulika zimegundulikana huko Baghdad zikiwa na majeraha ya risasi na alama zenye kuonyesha mateso waliyoyapata marehemu kabla ya kuuwawa.

Bado hali wasi wasi imetanda katika kitongoji cha Washia cha Sadr City kutokana na jeshi la Marekani kuzizingira baadhi ya sehemu za Iraq kufuatia mwanajeshi mwenzao kutekwa nyara wiki iliyopita.

Vizuizi hivyo vya jeshi la Marekani kumelekea Bunge la Iraq kuakhirisha kikao cha Bunge kilichokua kifanyike leo baada ya wajumbe 95 tu kuhudhuria kikao hicho kati ya wajumbe 275.

Wakati huo huo leo mchana mtu wa kujitoa muhanga akiwa na gari amejiripua katika sherehe ya arusi mjini Baghdad na kuwauwa watu 10 wakiwemo watoto na kuwajeruhi wengine 12.