1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Utulivu kupatikana baada ya miezi 12 hadi 18 kwa mujibu wa balozi wa Marekani nchini Irak

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzX

Balozi wa Marekani nchini Irak Zalmay Khalilzad amewahakikishia wapiga kura nchini mwake kuwa hali ya utulivu nchini Irak inaweza kufikiwa katika kipindi cha miezi 12 hadi 18 ijayo.

Akiwahutubia waandishi wa habari mjini Baghdad balozi Khalilzad ameelezea juhudi za kupambana na mauaji ya kimbari na wapiganaji wenye msimamo mkali nchini Irak ni changamoto kubwa kwa Marekani.

Balozi huyo amezilaumu Iran na Syria kwa kuunga mkono harakati za mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda unao endeleza machafuko nchini Irak na hivyo kuzuia lengo la Marekani la kutimiza demokrasia nchini humo.