1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Wanajeshi wa Marekani wapokelewa na mauaji ya watu zaidi ya 78 nchini Iraq

22 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYt

Zaidi ya watu 78 wameuawa na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa baada ya mambomu mawili kulipuka mfululizo katika soko la mitumba jijini Baghdad hii leo.

Polisi wamesema kuwa bomu la kwanza lililokuwa katika gari lilipuka katika eneo la wauza mitumba na wachuuzi wa bidhaa za mkononi kwenye soko la Bab al Sharqi, ambapo ni moja ya sehemu zenye watu wengi.

Dakika chache baadaye mtu wa kujitoa mhanga aliendesha gari lililokuwa na bomu la uzito wa kilo 100 na kujilipua katikati ya kundi la watu.

Vipande vya miili ya watu vimeonekana vimetapakaa kwenye madimbwi ya damu, huku moshi mweusi uliyosababishwa na milipuko hiyo ukigubika anga la eneo hilo.

Mauaji hayo yametokea muda mchache baada ya kundi la kwanza la askari elfu 3 wa ziada wa Marekani kuwasili Baghdad, wakiwa ni sehemu ya askari elfu 21 Rais George Bush aliyoahidi kuwapeleka Iraq.