1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.wapiganaji 18 wauwawa

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVp

Jeshi la Marekani nchini Irak limesema kuwa limewauwa wapiganaji 18 katika mji wa magharibi wa Ramadi.

Msemaji wa jeshi amesema zoezi hilo lilianza tangu jana mara tu wapiganaji walipowafyatulia risasi wanajeshi wa Marekani.

Kwengineko idadi ya watu waliouwawa kufuatia shambulio la mabomu mawili katika eneo la soko mjini Hilla imeongezeka kutoka watu 60 hadi watu 73 kufikia sasa.

Watu wengine 160 walijeruhiwa katika shambulio hilo.