1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Watu 30 wameuwawa nchini Irak

13 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCje

Mapigano mapya nchini Irak yamesababisha vifo vya takriban watu 30. Katika mji mkuu wa Baghdad pekee watu 15 wameuwawa kufuatia mashambulio ya mabomu katika maeneo yanayokaliwa na jamii ya Washia.

katika mji wa Al Hesna kusini mwa Baghdad watu waliokuwa na bunduki waliivamia nyumba moja ya familia ya Kishia na kuwauwa watu tisa wakiwemo wanawake na watoto watatu.

Nchini Marekani rais George W Bush amesema kwamba atatangaza mpango mpya kuhusu Irak mapema mwaka ujao kinyume na ilivyo tarajiwa hapo awali kuwa angetangaza wakati wa sikukuu ya krismasi.

Rais Bush katika mji wa Washington amefanya mazungumzo na makamanda wake wa kijeshi na pia katika mkutano mwingine ameshauriana na makamu wa rais wa Irak Tareq al Hashemi.

Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu ya White House ni kwamba rais Bush alitaka kupata taarifa zaidi kabla ya kufanya uamuzi wa mpango mpya wa Irak. Juu ya hali ya usalama wa Irak makamu wa rais wa nchi hiyo Tareq al Hashemi amesema.

O ton…….Huu ni wakati mgumu kwa raia wa Irak lakini kuna nuru inayojitokeza na kwamba kuna matumaini ya kufanikiwa, ijapokuwa tunahitaji kuwa na mioyo migumu na tuzidishe jitihada.