1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Watu kumi wameuwawa kwenye operesheni ya kijeshi

28 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLy

Takriban watu kumi wameuwawa kufuatia operesheni ya kikosi cha polisi cha Irak kikisaidiwa na helikopta za jeshi la Marekani.

Watu kumi na mbili wamejeruhiwa katika operesheni hiyo baada ya jengo moja kushambuliwa na vikosi hivyo kusini magharibi mwa Baghdad leo hii.

Maafisa wa Irak wamearifu kwamba shambulio hilo lilifanyika mapema leo na kuharibu makaazi ya familia moja ambayo ilikuwa usingizini.

Jeshi la Marekani halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na mkasa huo.

Kwingineko jeshi la Marekani limesema litaanzisha uchunguzi kufuatia tukio jingine ambalo maiti za watoto wanne na wanawake watano zimepatikana baada ya vikosi vya Marekani kufanya mashambulio katika kijiji kimoja mapema wiki iliyopita.