1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:watu zaidi ya 32 wauwawa Iraq

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5h

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameua zaidi ya watu 32 katika shughuli ya mazishi ya washia kaskazini mwa Baghdad.

Polisi ya Iraq imesema shambulio hilo limetokea ndani ya tenti iliyokuwa imejaa watu kwenye mji wa Khalis katika mkoa tete wa Diyala.Zaidi ya watu 60 walijeruhiwa.

Wakati huo huo jeshi la Marekani limefahamisha kwamba wanajeshi wake wanne waliuwawa mjini Baghdad mwishoni mwa juma na kuifanya idadi ya wanajeshi wa kimarekani waliouwawa Iraq mwezi wa April pekee kuwa zaidi ya 100.

Idadi hiyo imeufanya mwezi April kuwa mbaya kabisa kwa wajeshi hao wa Marekani tangu walipofavamia Iraq mwaka 2003.

Hadi sasa zaidi ya wanajeshi 3,300 wa Marekani wameuwawa Iraq.

Taarifa nyingine zinasema mkuu wa jeshi la Uingereza amesema Prince Harry atapelekwa Iraq kuungana na wanajeshi wengine mwezi ujao licha ya hofu kwamba wapiganaji wanaweza kulenga mashambulio yao dhidi yake.

Suala hilo lakini bado linajadiliwa.