1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Waziri Mkuu wa Iraq ziarani Iran

8 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBb7

Waziri Mkuu wa Iraq, Nour al Maliki anatarajiwa kuwasili Tehran hii leo katika ziara yake nchini Iran yenye nia ya kutafuta suluhisho la kiusalama nchini mwake.

Ziara hiyo ya Nour al Maliki inakuja siku chache tu baada ya wanadiplomasia wa Iran na Marekani kuwa na mazungumzo mjini Baghdad yenye kulenga kutafuta amani nchini Iraq.

Aidha ziara hiyo inakuja mnamo wakati ambapo serikali ya Waziri Mkuu huyo wa Iraq inakabiliwa na shinikizo kubwa la ndani na nje.

Iran na Iraq zilipigana vita ya miaka minane katika miaka ya 80, lakini uhusiano kati ya jamii ya washia wa Iran na wale wa Iraq wanaounda sehemu kubwa ya serikali ya Iraq umekuwa ukiongezeka.

Waziri huyo Mkuu wa Iraq anatokea Uturuki ambako alikuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.

Katika ziara hiyo viongozi hao walikubaliana kufanyakazi pamoja kukisambaritisha kikundi kilichojitenga cha wakurdi huko kaskazini mwa Iraq.

Uturuki kwa muda mrefu imekuwa ikiitaka Iraq kuwasambaratisha wanachama wa kikundi cha PKK ambacho kinachokuliwa kama cha kigaidi.