1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Waziri Mkuu wa Uingereza azuru Iraq

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKr

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amewasili nchini Iraq ambako anakutana na majeshi ya nchi hiyo yaliyoko huko pamoja na wabunge, ikiwa ni siku chache kabla ya kutangaza iwapo atapunguza majeshi yake nchini humo au la.

Mara baada ya kuwasili waziri mkuu huyo wa Uingereza alikwenda moja kwa moja kuonana na Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al Maliki.

Viongozi hao katika mazungumzo yao wanatarajiwa kujadili muda wa majeshi ya Iraq kukabidhiwa sehemu ya kusini ya jimbo la Basra ambalo liko chini ya majeshi ya Uingereza.

Hii ni ziara ya kwanza ya Gordon Brown nchini Iraq toka alipochukua kiti cha Uwaziri Mkuu wa Uingereza

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza anatarajiwa kulihutubia bunge mjini London wiki ijayo juu ya majaaliwa ya ushiriki wa Uingereza nchini Iraq.