1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bahrain. Bahrain wapiga kura.

26 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpJ

Upigaji kura umemalizika katika taifa la Bahrain katika eneo la ghuba, huku vyama vya upinzani vya Washia walio wengi vikishiriki katika uchaguzi huo wa taifa kwa mara ya kwanza tangu kususia uchaguzi wa mwaka 2002.

Baadhi ya makundi ya Washia wanadai kuwa kumekuwa na udanganyifu katika upigaji kura, lakini maafisa wa tume ya uchaguzi wamekana madai ya wizi wa kura na kusema kuwa wale ambao wanashaka na uchaguzi huo bila ya kutoa ushahidi wataadhibiwa.