1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAIDOA:Serikali ya mpito na mahakama za kiislamu wakubali kurudi kwenye mdahalo

21 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChY

Serikali ya mpito ya Somalia na viongozi wa mahakama za kiislamu wamekubaliana kuanza mazungumzo ya amani hayo ni kwamujibu wa mjumbe wa Umoja wa Ulaya.

Taarifa hizo zimekuja baada ya hapo jana kuzuka mapigano makali karibu na ngome ya serikali ya mpito mjini Baidoa ambapo serikali ya mpito ilidai ushindi kwenye mapigano hayo.

Baada ya kukutana na pande zote mbili Mjumbe wa umoja wa Ulaya Louis Michel alisema kila mmoja yuko tayari kuanza tena mazungumzo hayo bila masharti na kukubaliana kukomesha mapigano.

Lakini wakati mjumbe huyo wa ulaya akifanya mazungumzo na serikali ya mpito mjini Baidoa mapigano yalikuwa yakiendelea kilomita chache kutoka mji huo.