1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Balotelli awaambia wakosoaji wafyate midomo

21 Machi 2015

Mshambuliaji wa kilabu ya Liverpool ya Uingereza anayefahamika kwa visanga vyake Mtaliani mwenye asili ya Afrika Mario Balotelli amewashambulia wanaomkosoa akiwaambia " wafunge midomo."

https://p.dw.com/p/1EusA
Mario Balotelli Liverpool
Picha: imago/BPI

Akizungumza moja kwa moja kwenye kamera ya video aliyoiweka kwenye mtandao wake, Balotelli aliuliza, "mnanijuwa ?" mliwahi kuzungumza nami binafsi ?, mnajua niliyoyapitia katika maisha yangu ? Mmeniona tu nikicheza mpira uwanjani. Kwa hiyo fungeni midomo yenu." Akamalizia kwa ujumbe wa maandishi,uliosema," kwa wale waohukumu haraka haraka bila kujuwa kuhusu wengine." USIKU MWEMA.

Huenda mchezaji huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 24, alikuwa akijibu lawama dhidi yake kuhusu kiwango cwashake cha soka tangu alipowasili uwanja wa Anfieldo kujiunga na Liverpool ya Uingereza kutoka AC Milan ya Italia kwa kitita cha pauni milioni 16 sawa na euro zipatazo milioni 22.1 Agosti mwaka jana. Kusajili kwake kwa sehemu kulimfungulia njia Luis Suarez kuhamia Barcelona ya Uhispania. Balotelli amefunga magoli manne katika jumla ya mechi 20 katika mashindano yote na ameuona wavu mara moja tu katika ligi kuu ya England Premier League.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, rtre, afp
Mhariri: Saumu Yusuf