1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Balozi wa Pakistan nchini Afghanistan apotea

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6OP

Maafisa nchini Pakistan wanaongeza juhudi za kumtafuta balozi wa nchi hiyo nchini Afghanistan ambaye hajulikani aliko.

Inahofiwa mwanadiplomasia huyo alitekwa nyara katika eneo moja ambako wanamgambo wa Taliban wanaendeleza harakati zao.

Balozi Tariq Azizuddin pamoja na dereva wake walikuwa wakisafiri kuelekea mji mkuu Kabul jana Jumatatu,wakati walipopotea katika wilaya ya Khyber.

Maafisa wa usalama wanasema viongozi wa kikabila wanalisaka eneo hilo la milimani, linaloiunganisha Afghanistan na Pakistan, na wameifunga barabara kati ya nchi hizo mbili.

Mapema mwezi huu raia wawili wa Pakistan wafanyikazi wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu walipotea katika eneo hilo. Kufikia sasa hatima ya wahanga hao haijulikani.