1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAMAKO.Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi kutangazwa leo

30 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC5t

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa rais uliofanyika hapo jana nchini Mali yanatarajiwa kutangazwa hii leo.

Wananchi wa mali walipiga kura ambapo inatarajiwa rais Amadou Toumani Toure atachaguliwa tena kwa kipindi cha pili cha miaka mitano ikulu.

Waangalizi wa kimataifa wanasema uchaguzi ulifanyika kwa njia ya amani na utaratibu mzuri.

Toure alinyakua madaraka mwaka 1991 baada ya kufanya mapinduzi lakini baadae akaachia madaraka kwa rais aliyechaguliwa na raia.

Alirudi tena kwenye ulingo wa siasa kwa kushinda uchaguzi wa rais mwaka 2002.

Miongoni mwa wagombea wengine saba katika kinya’nga’nyiro hicho ni mwenyekiti wa baraza la kitaifa na waziri mkuu wa zamani Ibrahim Boubacar Keita.