1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban adai waasi wa M23 walisaidiwa kutoka nje

Josephat Nyiro Charo21 Februari 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amerudia tena shutuma kwamba waasi wa kundi la M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekuwa wakipokea msaada kutoka nje.

https://p.dw.com/p/17iet
UN chief Ban Ki-moon speaks during a press conference in Ankara, on December 7, 2012. UN chief Ban Ki-moon said on December 7 the use of chemical weapons by Syrian President Bashar al-Assad to combat the revolt would be an 'outrageous crime'. The UN chief, who flew to Turkey after visiting Jordan early Friday, repeated that he had written a letter to Assad urging him 'not to use under any circumstances chemical weapons' and warning him that 'it will create huge consequences.' AFP PHOTO/ADEM ALTAN (Photo credit should read ADEM ALTAN/AFP/Getty Images)
Ban Ki-moon in der TürkeiPicha: AFP/Getty Images

Katika ripoti yake kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa aliyoiwasilisha, Ban Ki Moon, hakutaja nchi yoyote inayowaunga mkono waasi wa kundi la M23, walioudhibiti kwa muda mfupi mji wa Goma, mnamo mwezi Novemba mwaka jana. Lakini wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamewahi kusema kwamba waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda na Uganda na Ban amesema nchi hizo mbili ziliwasijili watoto kuwa wanajeshi. Rwanda na Uganda zimekanusha vikali kuhusika na uasi dhidi ya serikali ya Kongo.

Wanajeshi wa serikali na wale wa tume ya amani ya Umoja wa Mataifa, MONUSCO, walifaulu kulizima shambulizi la kwanza la waasi wa M23 dhidi ya mji wa Goma, lakini Ban amesema shambulizi la pili lilidhihirisha wazi ushahidi wa msaada kutoka nje.

Congolese M23 rebels withdraw on December 1, 2012 from the city of Goma in the east of the Democratic Republic of the Congo. Hundreds of Congolese M23 rebels began a withdrawal on December 1 from Goma as promised under a regionally brokered deal, after a 12-day occupation of the city. Around 300 rebels, army mutineers who seized Goma last week in a lightning advance, were seen by an AFP reporter driving in a convoy of looted trucks north out the main town in Democratic Republic of Congo's mineral-rich east. AFP PHOTO/PHIL MOORE (Photo credit should read PHIL MOORE/AFP/Getty Images)
Waasi wa M23 mashariki mwa KongoPicha: Phil Moore/AFP/Getty Images

Ripoti inasema kasi, ustadi na ufanisi wa shambulizi la pili la waasi hao lililofaulu kutokana na kuongeza ghafla idadi ya wapiganaji, mashambulizi kadhaa ya muda yalipongwa barabara, na mashambulizi yaliyoratibiwa vizuri kati ya wapiganaji wa ardhini na washambuliaji wa risasi, haya yote yalionyesha uwezo ambao kundi hilo halikuwa nao hapo kabla.

Ripoti pia inasema usimamizi wa vikosi vya mashambulizi, jinsi vilivyosaidiwa na uratibu wa mashambulizi ya risasi, na ubora wa silaha na uwezo wake jumla wa kupigana, hasa wakati wa usiku, yote yalipendekeza kuwepo kwa msaada kutoka nje ya nchi, wa moja kwa moja na hata kupitia njia nyingine.

Usajili wa watoto jeshini

Ripoti ya Ban ilisema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda ziliwasajili watoto kuwa wanajeshi. Jumla ya vijana 21, wakiwemo takriban saba raia wa Rwanda wanaohusishwa na kundi la M23 katika mkoa wa Kivu Kaskazini, walihojiwa na tume ya MONUSCO. Ushahidi wao ulionyesha wazi dhahiri shahiri kampeni pana inayoendelea kwa mpangilio ya kuwasajili watoto walio na umri chini ya miaka 18 katika ardhi ya Kongo na Rwanda. Walizungumzia pia kuhusu watoto kuuwawa na kukatwa viungo katika kundi la M23.

Ripoti imewasilisha wakati kukiwa na mkataba wa kusitisha mapigano mashariki mwa Kongo huku Umoja wa Mataifa ukipanga kuimarisha kikosi chake cha kulinda amani katika eneo hilo.

Mkataba kusainiwa Addis

In this Wednesday Nov. 21, 2012 photo released by Uganda's Presidential Press Services, Uganda's President Yoweri Museveni, center, sits with his counterparts Paul Kagame of Rwanda, left, and Joseph Kabila of Congo during a meeting in Kampala, Uganda. The three heads of the states want the M23 rebels out of Goma, a town they captured from Congo army. (Foto:Presidential Press Services/AP/dapd)
Rais Kabila (kulia), Museveni na KagamePicha: dapd

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, anatarajia kusaini mkataba utakaomaliza machafuko baadaye mwezi huu. Rais wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo, Joseph Kabila, rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, wanatarajiwa kukutana mjini Addis Ababa, Ethiopia Jumapili ijayo kusaini makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa, yenye lengo la kumaliza miongo miwili ya vita mashariki mwa Kongo. Maraia wa Burundi, Angola, Afrika Kusini na Tanzania, watahudhuria pia mkutano huo.

Marais hao watasaini taarifa kuahidi kutoingilia masuala ya nchi jirani, huku Umoja wa Mataifa ukipanga kupeleka kikosi cha wanajeshi 2,500 mashariki mwa Kongo, kikiwa na amri ya kumaliza kitisho kutoka kwa waaasi wa M23.

Mwandishi: Josephat Charo/AFPE/REUTERS

Mhariri: Saumu Yusuf