1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki moon asema apata uungwaji mkono wa Gaddafi juu ya Darfur

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRd

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amesema amepata uungwaji mkono wa hali ya juu kutoka kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi juu ya kuutatua mgogoro wa jimbo la Darfur nchini Sudan.

Ban Ki-Moon aliyasema hayo baada ya kukutana na Muammar Gaddafi nchini Libya.

Ingawa Gaddafi hakuzungumza na waandishi wa habari lakini katibu mkuu wa Umoja wa mataifa alisema kiongozi huyo wa Libya ameahidi kutumia ushawishi wake kuyakutanisha makundi ya waasi ya Darfur nchini Libya kwa ajili ya mazungumzo na serikali ya mjini Khartoum mwezi ujao yanayosimamiwa na Umoja wa mataifa.

Libya kilikuwa kituo cha tatu cha katibu mkuu baada ya kuzitembelea Sudan na Chad katika ziara yake iliyokuwa na lengo la kuanzisha tena mazungumzo ya amani ya jimbo la Darfur.