1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki-moon kwenda Pakistan kuwaona wahanga wa mafuriko

Sekione Kitojo14 Agosti 2010

Mtu wa kwanza anayeugua ugonjwa wa kipindupindu ameripotiwa nchini Pakistan kufuatia mafuriko mabaya kuwahi kutokea nchini katika miaka kadha.

https://p.dw.com/p/OngF
Walionusurika na mafuriko nchini Pakistani wakipambana kupata mahitaji yanayotolewa na jeshi la nchi hiyo.Picha: AP

Islamabad.

Mtu  wa  kwanza  anayeugua  ugonjwa  wa  kipindupindu ameripotiwa   nchini  Pakistan  kufuatia  mafuriko  mabaya kuwahi  kutokea  nchini  humo  katika  miaka  kadha. Katibu  Mkuu  wa  Umoja  wa  Mataifa  Ban Ki-moon , ambaye  anatarajiwa   kuwasili  nchini  Pakistan  mwishoni mwa  juma  hili, ameonya  kutokea  wimbi  la  pili  la  vifo kutokana  na  magonjwa. Ban  anatarajiwa  kukutana  na wahanga  pamoja   na  mashirika  ya  kutoa  misaada. Mkuu  wa  shirika  la  kimataifa  la  msalaba  mwekundu Pascal  Cuttat  amesema.

Mkuu  wa  masuala  ya  kiutu   wa  Umoja  wa  Mataifa anayemaliza  muda  wake  John Holmes  ametoa  wito  wa kupatiwa  kiasi  cha  dola  milioni  460  za  msaada  wa dharura. Zaidi  ya  dola  milioni  100  zinahitajika   kwa   ajili ya   kuwahifadhi  mamilioni  ya   watu  ambao  hawana makaazi. Pakistan  na  Umoja  wa  Mataifa  zinakadiria kuwa   zaidi  ya  watu  milioni  13  wameathirika  na  maafa hayo  ambayo  yamesababisha  vifo  vya  zaidi  ya  watu 1,600.