1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban-Ki moon ziarani Sudan Kusini

Admin.WagnerD25 Februari 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon yuko mjini Juba kujaribu kufufua makubaliano ya amani ambayo mpaka sasa yameshindwa kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini, vilivyodumu kwa miaka miwili.

https://p.dw.com/p/1I2O4
KAtibu Mkuu Ban Ki-Moonkatika ziara yake ya awali nchini Sudan Kusini.
Katibu Mkuu Ban Ki-Moonkatika ziara yake ya awali nchini Sudan Kusini.Picha: Reuters

Katibu Mkuu Ban alipokelewa katika uwanja wa ndege ya Juba na waziri wa mambo ya nje Barnaba Maria Benjamin kabla ya kupelekwa kuonana na rais Salva Kiir, ambaye mgogoro wake na hasimu wake Riek Machar ulisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe Desemba 2013.

Mapigano yanaendelea licha ya makubaliano ya amani ya mwezi Agosti, ambap watu wasiopungua 18 wameuawa katika tukio la karibuni katika mji wa kaskazini-mashariki wa Malakal wiki iliyopita, wakati wanajeshi wa serikali waliposhiriki katika shambulizi dhidi ya kambi ya Umoja wa Mataifa iliyo na raia karibu 50,000 wanaotafuta hifadhi kutokana na vita hivyo.

Makubaliano ya Agosti, yaliyosainiwa chini ya shinikizo la kimataifa, yanamuacha Kiir akiwa rais na kumrudisha Machar katika nafasi yake ya zamani ya makamo wa rais, lakini katika ishara ya kiwango cha kutoaminiana kati ya wawili hao, Machar anaendelea kuishi uhamishoni licha ya kuteuliwa mapema mwezi huu.

Mahasimu wa Sudan Kusini - Rais Salva Kiir (kulia) na makamu wake Riek Machar (kushoto).
Mahasimu wa Sudan Kusini - Rais Salva Kiir (kulia) na makamu wake Riek Machar (kushoto).Picha: picture-alliance/AP Photo/P. Muller

Mapigano ya kuwania udhibiti wa nchi hiyo yameipeleka Sudan Kusini mara kwa mara katika kingo za kukumbwa na ukame, ambapo mamilioni ya raia wa nchi hiyo wamekuwa wakinusuriwa na baa la nja na uingiliaji wa mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa.

Ukiukaji wa haki za binaadamu

Mgogoro huo umeshuhudia ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu na mashambulizi dhidi ya raia, huku watoto wakiuawa ama kusailiwa na makundi ya wapiganaji, wanawake na wasichana hutekwa katika kambi za ubakaji na kutumiwa kama watumwa wa kingono, matukio kadhaa ya mauaji ya kikabila, mashambulizi dhidi ya vituo vya Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa misaada.

Uchunguzi wa Umoja wa Afrika uliyochapishwa mwaka uliyopita ulibaini ushahidi wa watu kulaazimishwa kula wenzao na kuhitimisha uhalifu wa kivita umetendeka nchini humo. Ripoti kadhaa za umoja wa Mataifa pia zimebaini ushahidi wa kuwepo na uhalifu wa kivita.

Si Kiir wala Machar aliekabiliwa na vikwazo kwa matendo ya vikosi vya kijeshi vilivyo chini ya uongozi wao. Wakati wa ziara yake, Ban atatembelea kambi ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu Juba, ambayo inawahifadhi watu waliotoroka mapigano - wakiwa miongoni mwa zaidi ya milioni 2.3 waliolaazimika kuyakimbia makaazi yao tangu mapigano yalipoanza.

Kambi ya wakimbizi wa ndani ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Juba.
Kambi ya wakimbizi wa ndani ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Juba.Picha: DW / F. Abreu

Kuhusu vikwazo dhidi ya Kiir na Machar

Wakati huo huo, serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa kitisho cha Marekani kuiwekea vikwazo ikiwa makubaliani yatanshindwa kuheshimiwa kinapswa kuelekezwa kwa waasi badala ya rais. Msemaji wa Rais Kiir Ateny Wek Ateny, amesema kitisho hicho kinapaswa kuwalenga wale wanaouwekea vizuwizi mchakato wa amani...na kuongeza kuwa tatizo haliko kwa Kiir.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alisema siku ya Jumatano kuwa Kiir na Machar watakabiliwa na vikwazo binafsi iwapo watashindwa kutimiza wajibu wao katika utekelezaji wa makubaliano, na kuonya juu ya kile alichokiita "wakati muhimu kwa nusura ya Sudan Kusini."

Mwandishi: Iddi Ssessanga/rtre,afpe

Mhariri. Mohammed Khelef