1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGKOK: Katiba mpya yaidhinishwa Thailand

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXj

Wapiga kura nchini Thailand wameidhinisha katiba mpya iliyopendekezwa na jeshi.Hiyo ni kwa mujibu wa waziri mkuu Surayud Chulanont.Kuambatana na matokeo ya mwanzo ya kura ya maoni iliyopigwa kote nchini,theluthi mbili ya wapiga kura wameunga mkono katiba iliyopendekezwa.Matokeo ya mwisho yanatazamiwa kutangazwa siku ya Jumatatu. Tangu Septemba 19,Thailand inaongozwa na serikali ya mpito iliyoundwa na baraza la wanajeshi,baada ya kupinduliwa kwa waziri mkuu wa zamani,Thaksin Shinawatra.