1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bangkok. Matumizi ya teknolojia yanaweza kupunguza ujoto duniani.

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4g

Wataalamu wa hali ya hewa kutoka mataifa 120 wamesema kuwa matumizi ya haraka ya teknolojia dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kupunguza kasi ya hali ya ujoto duniani, wakionya kuwa upunguzaji wa gesi zinazochafua mazingira unapaswa kuwa wa kiwango cha juu na kuanza kufanya kazi ifikapo 2015.

Ripoti ya hivi sasa ya jopo la umoja wa mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, iliyoidhinishwa baada ya mazungumzo ya siku tano, inasema kuwa kuacha hali ya joto kupanda kwa nyuzi joto mbili, itagharimu kiasi cha asilimia 0.12 cha uchumi wa dunia.

Makundi ya kimazimgira yamesifu ripoti hiyo kuwa kama ushindi kwa sayansi dhidi ya siasa.

Marekani, nchi ambayo inachafua mazingira kwa hali ya juu kabisa duniani , imesema kuwa pia inaidhinisha ripoti hiyo. Urekebishaji wa hali ya hewa ni pamoja na matumizi mazuri ya nishati kwa kutumia taa za umeme zinazotumia nishati kidogo, matumizi ya vyanzo kama upepo, nguvu za jua na mafuta ya asili, hadi katika vyanzo vyenye utata kama nishati ya kinuklia na uhifadhi wa carbon dioxide aridhini. Ujerumani ambayo inakuwa mwenyeji wa mkutano wa mataifa manane yenye viwanda duniani G8 Juni mwaka huu, imesema kuwa ripoti hiyo ni muhimu.