1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGKOK: Watu wawili wauwawa kwenye mashambulio ya mabomu

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCeL

Watu wawili waliuwawa na wengine 30 miongoni mwao watalii sita, wakajeruhiwa katika wimbi la mashambulio ya mabomu mjini Bangkok nchini Thailand.

Mabomu sita yaliripuka katika maeneo mbalimbali ya mji huo wakati watu walipokuwa wakijiandaa kuukaribisha mwaka mpya. Mabomu mengine mawili yalilipuka saa chache baadaye katikati ya jiji.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mashambulio hayo lakini polisi wanaamini yamefanywa na wamanamgambo kutoka eneo la kusini mwa Thailand.