1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bangkok

Oumilkher Hamidou30 Novemba 2008

Serikali yatishia kuwakamata na kuwatoza faini wafuasi wa upande wa upinzani

https://p.dw.com/p/G6JN

Bankok

Mvutano kati ya wafuasi wa serikali na wapinzani wao yanatishia kuzidi makali.Wafuasi 20 elfu wa chama tawala cha PPP wameandamana hii leo dhidi ya wapinzani wa chama cha "Muungano kwaajili ya demokrasia -PAD.Wanatishia kuivamia mahakama ya katiba iliyoamua jumanne iliyopita kuhusu uwezekano wa kuvunjwa chama cha PPP kutokana na udanganyifu uliofanyika wakati wa uchaguzi wa bunge mwaka mmoja uliopita.Leo asubuhi watu 50 walijeruhiwa guruneti liliporipuliwa karibu na makao makuu ya serikali.Wafuasi wa upande wa upinzani wa PAD wanaendelea kuvikalia viwanja vyote viwili vya ndege mjini Bankok.Baada ya njama ya kuyavamia majengo hayo kushindwa jana,serikali  inatishia hivi sasa kuwafunga na kuwatoza faini wale wote watakaodharau sheria ya hali ya hatari.