1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGKOK:Thailand yapata waziri Mkuu mpya,Jenerali Surayud Chulanont

1 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD78

Watawala wapya wa kijeshi nchini Thailand wametangaza katiba mpya ya muda ambayo pia imeungwa mkono na mfalme Bhumibol.

Watawala hao pia wamemteua Jenerali Surayud Chulanont kuwa waziri mkuu mpya.

Lakini jeshi litakuwa na mamlaka ya kumfukuza kazi waziri mkuu huyo endapo itabidi.

Jeshi pia litaendelea kudhibiti sehemu kubwa ya mamlaka hadi hapo uchaguzi utakapofanyika mwaka kesho.

Jenerali Sarayud Chulanont mwenye umri wa miaka 62 ni ascari jarabati anaeheshimiwa na jeshi na raia.