1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGKOK:Thaksin Shinawat afikishwa mahakamani

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpn

Waendesha mashitaka nchini Thailand, wamemfungulia
rasmi mashitaka ya rushwa , Waziri mkuu
aliyeangushwa Thaksin Shinawatra. Ni kesi ya kwanza
dhidi ya waziri mkuu huyo wa zamani kufikishwa
mahakamani, tangu alipopinduliwa na wanajeshi mwezi
Septemba mwaka jana. Mashitaka hayo dhidi ya Bw
Thaksin na mkewe yanahusika na ununuzi wa ardhi wa
kutatanisha mwaka 2003. Bw Thaksin amekana madai
hayo akisema ni njama ya kisiasa.Tangu
kuangushwa kwake anaishi uhamishoni mjini London.