1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGKOK:Wanasiasa wa serikali ya zamani walaumiwa kwa mashambulio ya mabomu

2 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdz

Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Thailand, jenerali Sonthi Boonyaratglin, amewalaumu wanasiasa wa serikali ya waziri mkuu Thaksin Shinawatra iliyoondolewa madarakani, kwa mashambulio ya mabomu yaliyofanywa mjini Bangkok usiku wa kuamkia mwaka mpya.

Akionya kuhusu uwezekano wa kutokea tena mashambulio mengine, jenerali Sonthi aliwaambia waandishi wa habari hapo jana kwamba wanasiasa wa upinzani wanataka kuusambaratisha usalama wa kitaifa na uchumi wa Thailand.

Watu watatu waliuwaawa na wengine zaidi ya 30, wakiwemo watalii tisa wa kigeni, kujeruhiwa katika milipuko minane ya mabomu.

Kupitia wakili wake, waziri mkuu wa zamani, Thaksin amekanusha madai ya kuhusika katika mashambulio hayo.