1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bangladesh 2000 wafariki

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIlw

DHAKA

Siku 3 baada ya kimbunga kikali kabisa nchini Bangladesh,waokozi wanajitahidi kuwapatia misaada maalfu ya walionusurika na maisha ambao wamepoteza sasa maskani zao.

Inakisiwa si chini ya watu 2000 wameuwawa na wakuu wa Bangladesh wanasema idadi hiyo yaweza kupanda .Katika wilaya ya Jhoalokati pekee zaidi ya wanavijiji 500 wamehilikishwa na dharuba kali .

Helikopta za jeshi zimekuwa zikidondosha misaada ya chgakula na manuwari za kikosi cha wanamaji zimeanza nazo kuwapatia watu misaada katika mwambao wa pwani wa bangladesh.

Kimbunga Sidr kilivuma Bangladesh alhamisi usiku n a kuteketeza pia mazao yote muhimu muda mfupi kabla mavuno.

Umoja wa Ulaya umejitolea kuipa Bangladesh msaada wa Euro milioni 1.5 huku Ujerumani ikiahidi Euro laki 5 zaidi.