1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGUI : Watu 20 wapotezewa makaazi

6 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuU

Takriban watu 20,000 wamekimbia nyumba zao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wiki iliopita wakati jeshi lilipotia moto mamia ya nyumba baada ya waasi kumuuwa afisa mwandamizi wa serikali katika eneo hilo.

Eneo hilo la kaskazini magharibi la koloni la zamani la Ufaransa limeshuhudia wimbi la umwagaji damu katika kipindi cha miaka miwili iliopita kwa mashambulizi ya waasi na kujibu mapigo kwa vikosi vya serikali ambavyo huvitia moto maelfu ya vibanda viliojengwa kwa nyasi na udongo kwa kujaribu kuwatimuwa waasi.

Mashirika ya haki za binaadamu yanasema raia 290,00 kutoka kaskazini mwa nchi hiyo ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wamepotezewa makaazi yao kwa nguvu katika kipindi cha miezi 18 iliopita wakiwemo 78,000 waliokimbilia nchini Chad,Cameroon na Sudan.