1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barack Obama atimiza mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani

4 Novemba 2009

Kuchaguliwa Barack Obama kama rais wa arobaini na nne wa Marekani mwaka mmoja uliopita, siku kama ya leo, lilikuwa ni tukio la kihistoria. Kwa mara ya kwanza mtu mwenye asili ya Kiafrika alikamata wadhifa wa juu wa dola.

https://p.dw.com/p/KO9P
President-elect Barack Obama, left, kisses his wife Michelle Obama after addressing supporters at the election night rally in Chicago, Tuesday, Nov. 4, 2008. (AP Photo/Jae C. Hong)
Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani hapo tarehe 4 Novemba,2008Picha: AP

Kuna watu wanaoutathmini kwa huruma mwaka huo, na kuna wale ambao wanasema nyota ya Obama iliokuwa inang'ara wakati wa kuchaguliwa sasa inaanza kufifia. Mfano hai ni matokeo ya jana katika uchaguzi wa magavana wa mikoa miwili ya Marekani, Virginia na New Jersey, ambako watetezi wa chama cha Democratic cha Rais Obama walishindwa na wale wa kutoka chama cha upinzani cha Republican.

Othman Miraji alimpigia simu Profesa Julius Nyang'oro, mhadhiri mwandamizi wa taaluma ya siasa katika Chuo Kikuu cha Mkoa wa Carolina ya Kaskazini, Marekani, kutaka tathmini yake kuhusu mwaka mmoja tangu kusikika vile vigelegele na nderemo zilizofuata kuchaguliwa Barack Obama kuwa rais wa Marekani.

Mtayarishaji:Othman Miraji

Mhariri: Mohamed Abdulrahman