1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barack Obama na Hillary Clinton nani ataibuka mshindi leo?

4 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DHgQ

TEXAS

Barack Obama na Hillary Clinton leo watapambana tena katika uchaguzi wa awali wa kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi wa atakayeshikilia bendera ya chama cha Demokratic katika uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani.Uchaguzi wa Leo kwenye majimbo ya Ohio na Texas untajwa kuwa huenda ndio utakaotoa picha halisi ya nani hasa atateuliwa kuwa mgombea wa chama hicho atakayepambana katika uchaguzi wa rais na mgombea wa chama cha Republican.McCain ambaye huenda akachaguliwa rasmi kuwa mgombea wa chama cha Republican anatazamiwa kupata wajumbe wakutosha kati ya wajumbe 250 ambao watagombaniwa kwenye majimbo ya Texas,Ohio,Vermont na Rhode Island dhidi ya mpinzani wake Mike Huckabee.MaCcain hadi sasa anaongoza katika chama cha Republican kwa kuwa na wajumbe 1014 kati ya wajumbe wote 1,191 wanaohitajika ili kuteuliwa rasmi kuwa mgombea wa urais wa chama hicho. Huckabee ana wajumbe 257 pekee.Kwa upande wa chama cha Demokratic wachambuzi wa mambo wanasema uchaguzi wa leo ni muhimu na hasa kwa Hillary Clinton ambapo itamlazimu ashinde.