1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza jipya la Mawaziri linasubiriwa kutangazwa nchini Kenya

7 Aprili 2008

Nchini Kenya baraza jipya la mawaziri bado linasubiriwa kutangazwa baada ya mazungumzo kuhusu ugawaji wa nyadhifa kugonga mwamba mwishoni mwa juma lililopita.

https://p.dw.com/p/DdXL

Hatua ya kuunda serikali ya mseto iliafikiwa baada ya muafaka kutiwa saini mwezi Februari kufuatia uchaguzi mkuu uliogubikwa na utata. Matukio hayo yalipelekea Rais Mwai Kibaki kuvunja safari yake ya India kunakofanyika mkutano wa kibiashara utakaowaleta pamoja viongozi kutoka mataifa mbalimbali wa bara la Asia na Afrika.

Kupata picha halisi ya mambo yanavyoendelea Thelma Mwadzaya alizungumza na mwandishi wetu wa Nairobi Mwai Gikonyo.