1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Mzozo wa Syria

Oumilkher Hamidou1 Februari 2012

Jumuia ya nchi za kiarabu imelisihi baraza la usalama lipitishe hatua dhidi ya utawala wa Syria,lakini Damascus na mshirika wake Urusi hawaonyeshi kuregeza kamba.

https://p.dw.com/p/13u4k
***Nicht für CMS Flash-Galerien verwenden*** A wide view of the Security Council in New York at its meeting on Kosovo-Serbia relations onm September 15, 2011. The meeting was called ahead of possible escalating tensions between Serbia and Kosovo over a border dispute. Photo Mark Garten/UN Photo
Baraza la Usalama la umoja wa mataifaPicha: picture-alliance/dpa

Wanachama 15 wa baraza la usalama,wengi wao wakiwa mawaziri wa mambo ya nchi za nje walimsikiliza mwakilishi wa jumuia ya nchi za kiarabu akiwasihi wapitishe azimio ili kumaliza "msiba" ulioangamiza maisha ya watu elfu tano tangu mwezi March mwaka jana.

"Hatushauri muingilie kati kijeshi...Hatuungi mkono utawala ubadilishwe,lakini tunapigania shinikizo la kiuchumi" amesema waziri mkuu wa Qatar,Cheikh Hamad ben Jassem Al Thani anaeongoza tume ya jumuia ya nchi za kiarabu kuhusu Syria.Amelalamika kwamba serikali ya Syria haionyeshi moyo wa kutaka kushirikiana kwa dhati,damu inazidi kumwagika na mauwaji yanaendelea.

Wakati baraza la usalama la umoja wa mataifa linaendelea na mjadala wake,nje karibu na jengo la taasisi hiyo muhimu ya kimataifa,wapinzani wa serikali ya Syria wamehanikiza kudai "Syria ikombolewe"

Demonstrators protest against Syria's President Bashar al-Assad in Jerjenaz, near Idlib January 27, 2012. Picture taken January 27, 2012. REUTERS/Handout (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Maandamano dhidi ya utawala wa rais Bashar al AssadPicha: Reuters

Licha ya miito ya jumuia ya nchi za kiarabu kutaka mswaada wao wa azimio kuhusu Syria uidhinishwe -Rashia na China zinaendelea kuupinga.Balozi wa Rashia katika Umoja wa mataifa Vitali Tschurkin anasema Umoja wa mataifa haustahiki kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyengine.

"Baraza la Usalama haliwezi kutoa muongozo utaratibu wa siasa ya ndani ya nchi unastahili uwe wa aina gani.Haijatajwa katika muongozo.Hatutaki kuona baraza la usalama likizoweya jambo hilo kwasababu tukianza tu,basi itakuwa shida kuzuwia;hapo litaanza kusema mfalme lazma ajiuzulu,waziri mkuu anabidi ajiuzulu-yote hayo hayalihusu baraza la usalama."

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton amekosoa ile hali kwamba baadhi ya wanachama wa baraza la Usalama wanahofia kitisho cha kutokea hali kama ile ya Libya."Hali hizi mbili hazilinganii "amesisitiza waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani.

U.S. Secretary of State Hillary Clinton (C) meets with French Foreign Minister Alain Juppe (R) and British Foreign Minister William Hague before a UN Security Council meeting at the United Nations in New York January 31, 2012. The Arab League will ask the U.N. Security Council on Tuesday to adopt a resolution endorsing an Arab plan for Syrian President Bashar al-Assad to transfer powers to his deputy. REUTERS/Mike Segar (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton (katio) na mawaziri wenzake,Alain Juppé wa Ufaransa (kulia) na William Hague wa Uengereza (kushoto)Picha: Reuters

Baraza la Usalama linatazamiwa kuendelea na majadiliano yake hii leo kuhusu mswaada uliofanyiwa marekebisho na ambao balozi Tschurkin anautaja kuwa "na baadhi ya mambo yanayotia moyo."

Mwishoni mwa kikao cha jana,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Alain Juppé alisema "kuna uwezekano wa kufikia maridhiano pamoja na Moscow" na hasa kuhusu hatima ya rais Bashar al Assad.

Waziri mwenzake wa Uingereza William Hague amezungumzia "majadiliano pamoja na Rashia na mataifa mengine katika kipindi cha masaa 24 yajayo .

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Afp/Reuters

Mhariri: Abdul-Rahman Mohammed