1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la usalama UN lahimiza msaada wa usalama kwa Haiti

15 Julai 2023

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, jana liliyahimiza mataifa kutoa msaada wa usalama kwa Haiti kwa kupeleka kikosi maalumu ambacho kiliombwa mwaka jana na serikali ya nchi hiyo ili kukabiliana na magenge ya uhalifu.

https://p.dw.com/p/4Twdg
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa MataifaPicha: Eskinder Debebe/UN Photo/Handout/Xinhua/picture alliance

Katika mkutano wake, baraza hilo la Umoja wa Mataifa, lilipitisha azimio la kurefusha kwa mwaka mmoja jukumu la ujumbe wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti. Azimio hilo pia liliunga mkono wito wa msaada wa usalama kwa polisi wa nchi hiyo.

Soma zaidi: Guterres atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuyapa kipaombele mahangaiko ya watu wa Haiti

Baraza hilo lenye wanachama 15, linayahimiza mataifa wanachama pamoja na  mataifa katika eneo hilo kutoa msaada wa kiusalama kwa jeshi la polisi la Haiti ikiwa ni pamoja na kupeleka kikosi maalumu. Pia limemtaka Guterres kuwasilisha ripoti kwa baraza hilo ndani ya siku 30, kwa kushauriana na Haiti, kuelezea kikamilifu aina ya misaada ya Umoja wa Mataifa.