1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la usalama lajadili vikwazo vipya dhidi ya Iran

29 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyzX

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeanza kujadili maswala yatakayojumulishwa katika azimio jipya linalonuiwa kuviongezea nguvu vikwazo dhidi ya Iran kwa kukataa kuachana na mpango wake wa nyuklia unaozozaniwa.

Wanachama watano wa baraza la usalama pamoja na Ujerumani, wamekuwa wakijadili vipengele muhimu vya azimio hilo, ikiwa ni pamoja na marufuku ya kusafiri, kuzifungia mali, madeni ya usafirishaji wa bidhaa, usimamizi wa fedha, uchunguzi wa mizigo na tarehe ya mwisho ambapo Iran itatakiwa iachane na mpango wake wa nyuklia.

Mawaziri wa kigeni wa Marekani, Urusi, Ufaransa, Uingereza, China na Ujerumani waliyatayarisha mapendekezo hayo wakati walipokutana wiki iliyopita mjini Berlin Ujerumani na kuyawasilisha kwa nchi 15 wanachama wa baraza la usalama mjini New York.

Jana hakukuwa na kikao rasmi cha baraza hilo lakini wanadiplomasia wanasema nchi wanachama zilikutana katika vikao mbalimbali.