1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dimba la Ulaya larejea kwa kishindo

Admin.WagnerD24 Novemba 2015

Champions League inarejea uwanjani Jumanne na Jumatano ambapo Barcelona na Bayern Munich zinaelekea kukata tikiti zao kuingia katika timu16 bora na Arsenal na Chelsea zikiingia katika michezo muhimu

https://p.dw.com/p/1HB1E
Spanien Fußball UEFA Champions League FC Barcelona - Bayern 04 Leverkusen Luis Suarez
Picha: Getty Images/A. Caparros

Bayer Leverkusen inatambua kuwa ina mchezo wa mwisho na Barcelona , na haitaki kufanya makosa dhidi ya mabingwa wa Belarus BATE Borisov. Leverkusen inayokamata nafasi ya tatu katika kundi E iko nyuma ya Roma kwa pointi moja lakini imeshindwa mara tatu msimu huu katika michezo ya nje.

Barcelona inapambana na Roma , ikiwania kukata tikiti yake na mapema katika timu 16 bora . Arsenal inapambana na Dinamo Zagreb na inalazimika kulipiza kisasi cha kufungwa katika mchezo wao wa kwanza ili kujihakikishia uhai wa kuendelea katika Champions League msimu huu.

Bayern Munich inakumbana na Olimpiakos Pireus na ikicheza nyumbani inauhakika wa kunyakua tikiti ya kucheza katika duru ijayo ya timu 16 bora.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre/dpae/ afpe
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman